Na Beatrice Kaiza 


Kampuni ya Wasafi media imezindua rasmi msimu wa tamasha la burudani la WASAFI FESTIVAL "Hii imeendaaa", 


Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Wasafi Media Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ leo August 7,2023 katika  Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam amesema  watatumia jukwaa hilo la Wasafi Festival 2023 kuelimisha vijana na kutoa ajira.


“WasafiFestival2023 itaanzia Mtwara, kwa mara ya kwanza Mtwara walitupokea kwa shangwe kubwa, rekodi kubwa, ukiacha kufanya show hata msanii wetu wa kwanza tulimpata Mtwara, kwa hiyo Mtwara ni kama nyumbani,” amesema Diamond.



Pia aliongezea kuwa usajili na utambulisho wa wasanii watakaotumbuiza kwenye Wasafi Festival 2023 utafanyika Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba, Jumamosi hii tarehe 12.



Aidha amesema Tamasha hilo litafanyika katika mikoa kumi ya Tanzania na pia wananchi watapata burudani,elimu na fursa za kibiashara kwa vijana na watanzania kwa ujumla.