Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka ameagiza Shule zote zilizopata fedha za ujenzi wa mabweni zifungwe camera za CCTV lengo likiwa ni kumarisha ulinzi na usalama wa Wanafunzi.



Mtaka ametoa agizo hilo alipotembelea na kukagua

Shule va Sekondari Yakobi wakati wa kuwapokea Wanafunzi wa kidato cha tano ambapo amesema kutokana na kuwapo kwa historia va ukiukwaii wa maadili ulioripotiwa Shuleni hapo Mkurugenzi wa

Halmashauri ya Mji wa Njombe pamoja na maeneo mengine wanapaswa kuchukua hatua za kufunga mifumo ya camera.

"Tuna Halmashauri sita, Watu wa TEHAMA na Watu wa TTCL wapite kwenye Shule ambazo pesa za mabweni zimetolewa waone namna ya kufunga miundombinu ya camera ili tuweze kuondokana na matukio ambayo wakati mwingine yamehatarisha

Watoto"

Afisa elimu Mkoa wa Niombe Mwalimu Nelasi

Mulungu amesema Serikali imetoa Tsh. bilioni 4.8 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni kwenye Shule 12 za

Sekondari na hivvo kila mmoja anapaswa kuchukua hatua za kumsaidia Mtoto.