Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaapisha Mabalozi Wateule Ikulu Chamwino Dodoma leo August 16,2023 ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba ni kwamba kuna Mabalozi ni kama vile hawajui wanachokifanya kwakuwa wapowapo tuna hawafanyi kazi kwa ufanisi.

"Katika Nchi nyingine Mabalozi wet sijui niseme hawajui wanachokifanya, wapo tu, nilishakutana na Rais mwenzangu ndani ya Nchi za Afrika, ndani ya

SADC akaniambia nibadilishie Balozi uliyeniletea hata kazini haendi, mikutano hashiriki yupoyupo tu hatuelewi, Tanzania hatujawazoea hivyo sasa labda ubadilishe nikamwambia nimekusikia"



"Lakini Mabalozi wengine unawaona pale ambapo

Ujumbe wa Tanzania umekwenda kwenye Nchi hiyo, au siku za kisherehe za Kitaifa za Nchi hiyo anakwenda kuwakilisha Nchi yake lakini mengine hakuna, au labda Watanzania wafanye ukorofi wakamatwe huko ndio utaona taarifa ya Balozi lakini vingine huoni"

"Sasa inawezekana pia labda na aina ya Mabalozi tunaowapeleka inawezekana, karibuni hivi nilitengeneza Kamati ipitie Wizara hi ya Mambo ya Nje iniletee kasoro zilizopo, nimepokea draft ya kwanza nimewarudishia wanaendelea kufanyia kazi nadhani ripoti itakapokuja itasaidia turekebishe

Wizara yetu"