Na Beatrice Kaiza


Kampuni ya Star Media (T) Limited kupitia chapa yake ya StarTimes wakishirikiana na BFC one pamoja na Quantum infinity wameandaa Pambano la Boxing siku ya Jumamosi Tar 29 Julai.


Katika siku hiyo kutakuwa na Mapambano zaidi ya 13 ikiwemo lile na kuwania mkanda wa UBO ambapo ABDUL UBAYA (Tanzania) atapambana dhidi ya IVAN MAGUMBA (Uganda) na kwa upande wa kuwania Mkanda wa WBC kutakuwa na Emmanuel Shija akipambana dhidi ya Yusuph Fundi wote hawa ni watanzania.


Akizungumza na waandishi wa habari Meneja masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa amesema kuwa mapambano yote haya yataruka mubashara kupitia chaneli yako pendwa ya TV3.


“Chaneli ya TV3 inapatikana katika kisimbuzi cha StarTimes, Kwenye Dishi  na  Antena.Kwa Mtumiaji wa Dish chaneli hii ni namba 197 katika kifurushi cha Smart(Tsh 21000/=) na mtumiaji wa antena chaneli hii ni namba 131 katika kifurushi cha Mambo(Tsh 15000/=).

Mwisho nipende kutoa wito kwa watanzania wote kwamba kipindi hiki sio cha kukosa kuangalia, Kama bado hauna kisimbuzi cha  StarTimes  wahi kwenye maduka yetu au wakala aliye karibu na wewe ukajipatie kisimbizi chako kwa bei ya punguzo, ambapo Dishi ni Tsh 79000/= chenye ofa ya kifurushi cha juu cha Tsh 36000/= bure kwa mwezi mzima. Vivyo hivyo kisimbuzi cha Antena pekee ni Tsh 42000/= kikiwa na ofa ya kifurushi cha juu cha Tsh 20000/= bure mwezi mzima amesema Malisa.