Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (Tawa), imeanza kutumia Panya waliopewa mafunzo maalum na Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), kudhibiti ujangili nchini.
Ofisa daraja la kwanza wa Tawa, Tryphon Kanon amesema hayo jana Alhamisi, Julai 20,2033 wakati akitoa mada kwenye semina ya wahariri iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (Jet), kwa ufadhilli wa mradi wa Tuhifadhi Maliasili unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani.
Kanon amesema panya hao wameshaanza kazi katika Bandari ya Dar es Salaaam na kwamba kwa kupekuwa mizigo yote ya abiria inayopita katika babdari hiyo sambamba wakisaidiana na mbwa na askari waliopewa mafunzo maalum.
“Kwa muda mfupi ambao panya hao wameanza kutumika katika bandari hiyo wamekuwa msaada mkubwa na matokeo yake yanaridhisha,” amesisisiza mtaalam huyo wa wanayamapori.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Jet, John Chikomo amesema ulinzi wa wanyama, uhifadhi na maliasili unategemea jamii zaidi hivyo kwa kuwaelimisha wahariri itasaidia kusambaza elimu hiyo.
Chikomo amesema wahariri wakielewa dhaba nzima ya uhufadhi wa maliasili watatoa fursa kwa habari, makala na kuandaa vipindi maalum vitakavyoelimisha jamii na kusababisha kulindwa kwa maslahi ya vizazi vijavyo.


