Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo anatarajja kupanda ulingoni kuwania mkanda wa Dunia wa WBO chini ya kampuni ya promosheni ya ngumi za kulipwa nchini PAF Promotion Entertainment ltd katika pambano litakalopigwa Agosti mwaka huu.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Hassan Mwakinyo alisema kuwa kwa sasa amejipanga kuhakikisha anakata kiu ya watanzania wanaopenda mchezo wa ngumi za kulipwa kwa kucheza pambano ambalo la mkanda ambao hajauwahi kuchezwa nchini.
"Baada ya kukosekana ulingoni katika ngumi za ushindani Hassan kwa muda mrefu,nawashukuru waandishi wa habari kwa kuja hapa natarajia kupanda ulingoni mwenzi ujao katika pambano kubwa la kuwania mkanda wa ubingwa wa Dunia wa WBO" Alisema Mwakinyo
Aidha amefafanua sababu ya kutoonekana ulingoni Mwakinyo alisema "Muda mrefu nilikuwa natamani nipate pambano kama hili lakini nilikuwa bado sina vigezo, sasa nashukuru nimefanikiwa kupata vigezo na utakuwa wakati mzuri kwangu kupata pambano hili;Ningefurahi pia kwa mabondia wa Tanzania wangepata na wao nafasi kama hii tena wakipigana hapa hapa nchini lakini bado vigezo hawana"
Mwakinyo aliongezea kuwa "Ukimya wangu haukuwa wa bure, nitakidhi kiu ya mashabiki wangu ambao hawajaniona muda mrefu ulingoni,Nitawasterehesha na kuwaburudisha mashabiki wangu, Nimejiandaa na bado najiaandaa vyema mpaka sasa kwa pambano hili"
"Kwa Tanzania Boxer yoyote anayetaka kupigana na mimi kwanza agombee mkanda huu ninaokwenda kuupigania lakini pia hata mabondia wakubwa huwa wanacheza sparling hivyo kama kuna bondia anataka hivyo aje masaki tupigane" alisema Hassan Mwakinyo

