Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions inayoandaa matamasha mbalimbali ya injili nchini, Alex Msama amewashauri viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge, kuwa bega kwa bega na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake anazofanya katika kuhakikisha uchumi wa nchi unakuwa.
Akizungumza mapema leo,Julai 6, 2023, na waandishi wa habari
amesema kuwa Wabunge pamoja na viongozi wengine wanapaswa kuwa imara katika kupeperusha sera nzuri za Tanzania na hawapaswi kubaki nyuma katika kuunga mkono jitihada za Rais Samia.
“Watu wote ambao wenye nia mbaya na nchi yetu, lazima tupambane nao bila kuwaogopa wala kuwaonea haya. Nchi yetu ni ya kila mtamzania, na ana haki ya kupambana kuhakikisha Amani, Utulivu na mshikamano tulionao unaendelea kuwepo.
“Rais anafanya kazi kubwa mambo mengi yalikuwa hayaendi, lakini sasa mambo yanaenda vizuri sana, wawekezaji wakubwa, wadogo na wa kati wanakuja kuwekeza nchini kwetu, haya yote ni matunda yatokanayo na yeye kutembelea kwenye Nchi mbalimbali za kigeni kuunganisha Biashara ili kukuza uchumi wa nchi” amesema Msama.

