Ikiwa imebaki siku moja kuelekea fainali ya Shindano la Miss Tanzania 2023 mapema leo zawadi ya Miss Tanzania imetambulishwa rasmi gari aina ya Mercedez Benz yenye thamani ya Sh Milioni 30 za kitanzania na pesa taslim Milioni 10.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Azama Mashango amesema kuwa zawadi ya Miss Tanzania itakuwa ni gari aina ya Mercedez Benz yenye thamani ya Sh Milioni 30 na pesa taslim ya Milioni 10.
“Mshindi wa 6 mpaka yule wa 20 atapata laki 2 kila mmoja, mshindi wa 5 na wa 4 ni Milioni 1 na mshindi wa milioni 2 mshindi wa pili Milioni 10,” amesema Mashango.
Aliongezea kuwa Ijumaa hii itakuwa ya historia kwani ndio mshindi wa Miss Tanzania 2023 atatangazwa rasmi na kuibuka kidedea na kuondoka na zawadi ya gari ya Mercedez Benz na pesa Milioni 10.
Pia fainali ya Miss Tanzania 2023 itafanyika katika ukumbi wa The Super Dome uliopo Dar es Salaam jijini Masaki.
Kwa upande wa Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa ameeleza kuwa watu walipie vifurushi vyao mapema.
“ Startimes ndio sehemu pekee na hakuna sehemu ingine ambayo utapata kuona fainali hii ya kukata na shoka zaidi na hapa St. Bongo mashabiki wa urembo wakae mkao wa kula,” amesema Malisa.

