KAMPUNI ya Azam Media leo imetambulisha tamthilia mbili zilizokuwa zikisubiriwa kwa muda mrefu zinazoitwa ‘Mtaa wa Kazamoyo na Lolita’ za Kitanzania.
Tamthilia hizo zilizobeba simulizi na kuleta mapinduzi ya tasnia ya tamthilia nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari, Msimamizi Mkuu wa Chaneli ya Sinema Zetu Sophia Mgaza amesema kuwa uzalishaji wa tamthia hizi mbili zimezingatia mahitaji ya soko kwani wametumia vifaa vya uzalishaji wa kisasa na ubora wa hali ya juu,” amesema Mgaza.
Aliongezea kwa kutoa rai jwa waandaaji wapya wanaongia na kaxi zao za sanaa zinazoruka kwenye chaneli hiyo waweze kuhakikishia wanasimamia ubora wa kazi ili wasije kutoa sababu kwa watu wa pembeni kuwanyooshea vidole na kusema kuwa ilikuwa ni nguvu ya soda tu,” amesema Mgaza.
Pia amesema kuwa Tamthilia hizo zinachukua nafasi ya Fungu langu itakayofikia tamati tarehe 29 Julai 2024 na Jeraha itakayofikia tamati tarehe 10 Agosti, 2023.

