Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi leo ameagana na  aliyekuwa mwakilishi Mkazi wa shirika la UNICEF nchini Tanzania Shalini Bahuguna Ikulu, Zanzibar. 


Aidha, Rais Dk.Mwinyi amemshukuru Shalini kwa ushirikiano aliyoipatia Zanzibar kwa kipindi cha Miaka minne alichokua akitimiza majukumu yake, hasa kwa kushiriki katika  ustawi na Maendeleo ya watoto nchini.




Kwa upande wake Bi. Shalin  amemshukuru Rais Dk.Mwinyi kwa ushirikiano, na kumpongeza kwa utendaji wake, kipindi chote walichokua wakishirikiana kuboresha hali za watoto nchini.


Katika kipindi chake cha Miaka minne Bi Shalini amefanikisha uboreshaji wa huduma za chanjo kwa Watoto chini ya miaka mitano, utoaji wa lishe bora  pamoja na kuimarisha mfumo wa huduma za dharura kwa ushirikiano na watoa huduma za afya ngazi ya jamii.