Rais Dk. Mwinyi katika safari hiyo ameambatana na Waziri wa Habari Vijana na Michezo Mhe. Tabia Mwita, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mbali na kushiriki uzinduzi wa Mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu jijini Berlin, Rais Dk, Mwinyi pia atakutana na viongozi wa juu wa Serikali nchini humo, Wakuu wa Mashirika mbalimbali, Wawekezaji na jamii ya Watanzania waishio Ujerumani (Diaspora).
