KLABU Ya Jeshi la Ulinzi La Wananchi Wa Tanzania(JWTZ )Lugalo Golf Kuoneshana Umwamba Wa Mchezo Wa Golf Na Klabu Ya  Dar Gymkhana Juni 03,2023 Dar es salaam.


Akizungumza Wakati Akiendelea na Maandalizi Ya Shindano La "CRDB INTER CLUB CHAMPIONSHIP" Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo Mwenyekiti Wa klabu Ya Jeshi Lugalo Gofu Amesema Lengo La Shindano hilo ni kudumisha Umoja Na Mshikamano Wa Klabu hizo na Kuendeleza Mchezo Wa Gofu Nchini Tanzania.


Pia ameongeza kuwa tayari washiriki 100 wamejisajili kushiriki shindano hilo linalotarajiwa kufanyika viwanja vya Lugalo Gofu .



Aidha Luwongo ameongeza kuwa kuwepo kwa shindano linaloshirikisha vilabu mbalimbali inasaidia hasa  kuwaweka karibu na kupeana mawazo mbalimbali katika kujenga mchezo wa gofu baina ya vilabu hivyo.


Pia ametoa wito kwa wachezaji na wadau mbalimbali wa michezo kujitokeza kutazama shindano hilo ambalo viongozi mbalimbali watahudhuria.






Kwa upande wake  Frank Laizer  Nahodha Wa Klabu Ya Dar Gymkhana Amesema Hamasa Ni Kubwa Kwa klabu hizo Ambazo Ndio Kinara Wa Mchezo huo Dar es salaam na chachu ya Kuendeleza Gofu  Hivyo Licha Ya Ushindani kuwa Mkubwa kwa Wachezaji wanaimani wataibuka na ushindi.






 "Tumepata watu wengi ambayo tayari wamejiandikisha Wachezaji  23 ambao kwa watu wawili wawili wanakamilisha idadi ya watu 46 na wanaendelea na maandalizi."








Pia ameeleza kuwa kwa muonekano wa mchezo na mipango ya klabu ya Gymkhana ilivyoweka ingependeza zaidi shindano kama hili liweze kufanyika mapema kwa kila baada ya miezi mitatu itasaidia kuhamasisha watu wengi wajiunge na mchezo huu.