Michezo ya mwisho ya Ligi Kuu Tanzania itafanyika Juni 9 badala ya Mei 28 mwaka huu ili kutoa nafasi kwa Yanga SC kucheza michezo ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Bodi ya Ligi imesema uamuzi huo umelenga kuweka usawa na kuondoa uwezekano wa kupanga matokeo.