Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo ameshiriki hafla ya utiaji saini mikataba ya miradi ya kufikisha huduma za mawasiliano ya simu katika kata 763 nchini, Jijini Dodoma na ametumia nafasi hiyo kuagiza Taasisi za Serikali kuondoa urasimu wa kutoa vibali vya ujenzi wa minara na ameagiza vibali vya minara iliyotiwa saini leo visifikishe mwezi mmoja.
Rais Samia amesema “Kuna changamoto kadhaa inabidi kama Serikali tuzitupie macho, kuna changamoto ya upungufu wa umeme Vijijini ambako minara inakwenda kujengwa, mnara mmoja kwa mwezi unatumia Mil 1.8 tukitumia jenereta lakini tukienda kwenye umeme tunaotumia wa gesi na maji tutatumia Tsh. Laki 4 tu kwa mwezi kwa mnara mmoja”
Kuna changamoto ya urasimu wa Taasisi mbalimbali katika utoaji wa vibali, Wizara imeniambia ili mnara usimame unachukua karibu miezi sita, sasa naagiza vibali hivi vya minara iliyosainiwa leo visizidi zaidi ya mwezi mmoja vibali vyote viwe vimetoka, June 13 nitamuuliza Waziri mmekwendaje, mmekwama wapi na nani kakwamisha!?”
