Na Beatrice Kaiza 


Balozi wa Tanzania nchini Cuba Hamfrey Polepole amefanya ziara katika kiwanda cha Tanzania Biotech Products Limited kilichopo Kibaha ambacho kiwanda  cha kimkakati na maabara kubwa ya Bioteknolojia kinachozalisha dawa ya viuadudu vya mbu na mazalia ya mbu, kiwanda hiki ni matokeo ya Tanzania na Cuba.

Balozi  Pole pole akiwa ameongozana na  Balozi wa Cuba nchini Tanzania  HE Amb,Yordenis Despaigne amesema wataakikisha dhumuni la kiwanda hiki kitafika malengo ya kutokomeza maralia2025_2030.

“Rais wetu Samia Suluhu Hassani hapendezwi na vifo vya ugonjwa wa maralia nchini Tanzania kwani kuna kiwanda tayari kipo cha kuakilisha kinaua mbu na mazalia yake nchini," amesema Polepole 

Ameongezea kuwa kiwanda hicho kinauwezo wa kutengeza  lita  Milioni sita kwa mwaka lakini wizara za afya kimetumia Lita laki nne Kwa mwaka"amesema Polepole

Pia ameliomba Bunge la bajeti kuweza kuweka fedha za kutosha katika wizara ya afya ili hatimae wizara ziweze kutumia dawa hizi na kuwasaidia wananchi wa Tanzania .