Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufuatia vifo vya Watu wawili kufuatia ajali ya ndege ya shirika la Frankfurt Zoological aina ya Cessna 182 na usajili wa namba 5H-FZS
Ajali hiyo imetokea 5:30 muda mfupi tu baada ya kuruka kutoka kwenye kiwanja kidogo cha Matambwe kwenye hifadhi ya taifa ya Nyerere, Ndege hiyo ilikuwa na abiria 3 na rubani 1.
Katika ajali hiyo askari wawili wamejeruliwa na hali zao sio nzuri ambapo baada ya kuokolewa walipokelewa katika zahanati wakisubiri ndege kupelekwa katika hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika zahanati hiyo, Rais Samia ametoa pole kwa familia za wafiwa na anaungana nao katika kipindi hiki cha majonzi.

