Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete wameongoza waombolezaji katika maziko ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe ambaye amezikwa kijijini kwake, Rondo, Chiponda mkoani Lindi.
Membe alifariki Ijumaa Mei 12, 2023 katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar e Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu baada ya kuugua gafla.
Kwa mujibu wa daktari wake binafsi, Profesa Harun Nyagori; kifo cha mwanasiasa huyo kimesababishwa na ugonjwa wa maambukizi ya mfumo wa mapafu hewa, ambao unasababisha mgando wa damu na kuzuia mapafu kupeleka hewa ya oksijeni.


